Mfumo wa Siasa

Mfumo wa Siasa wa Zanzibar ni Demokrasia ya vyama vingi vya siasa ambapo Rais wa nchi huchaguliwa baada ya kupigiwa kura na wananchi kutoka miongoni mwa wagombea wa vyama kadhaa vilivyoshiriki katika uchaguzi husika.

 

Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar ni Dk. Ali Mohamed Shein (CCM) tangu Machi 2016. Rais wa Zanzibar anachaguliwa katika kura ya moja kwa moja (direct popular vote) kwa kipindi cha miaka mitano mitano.

 

Mfumo wa Uchaguzi

Mfumo wa uchaguzi unaotumika katika kuchagua Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ni  wa mgombea anayepata kura nyingi kuwashinda wagombea wengine ndiye huwa mshindi (First Past The Post). Hata hivyo, sambamba na mfumo huo kuna asilimia 40 ya Viti Maalum Vya Wanawake wanaoingia katika Baraza la Wawakilishi na Udiwani kwa mlingano wa asilimia za kura za chama husika ambacho kimepata katika Uchaguzi Mkuu.

 

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lina Wajumbe 87, ambao 54 kati yao wanachaguliwa moja kwa moja katika majimbo ya uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika katika kila baada ya miaka mitano. Wajumbe wengine 10 wa Baraza hilo wanateuliwa na Mhe. Rais baada ya kukamilika kwa  Uchaguzi Mkuu, Wajumbe  22 wa Viti MaalumVya Wanawake wanaoteuliwa na Tume baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu kulingana na idadi ya asilimia ya kura ambazo kila Chama kimepata katika uchaguzi. Nafasi moja ya Uwakilishi inajazwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar kutokana na wadhifa wake. Wajumbe wote hao isipokuwa vyenginevyo hufanyakazi yao katika Baraza la Wawakilishi kwa kipindi cha miaka mitano. Wakuu wa mikoa ambao kwa nafasi zao walikuwa wanaingi katika Baraza la Wawakilishi kama Wajumbe wa Baraza hilo  si Wajumbe tena wa Baraza la Wawakilishi.

 

Bofya hapa kwa maelezo zaidi.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii