UCHAGUZI MKUU

Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania/Zanzibar kwa maelekezo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977 na Katiba ya Zanzibar, 1984 huendeshwa katika  kila baada ya kipindi cha miaka mitano na wapiga kura hupiga kura ya kumchagua Rais wa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Uchaguzi unaoendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 

Kwa uchaguzi unaoendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, mbali na  wapiga kura wa Zanzibar kumchagua Rais na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pia hupiga kura kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Barala la Wawakilishi  na Madiwani.   

Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uchaguzi Mkuu wa vipindi vya miaka mitano mitano ulianza tangu mfumo wa chama kimoja cha siasa ambapo wagombea wote wa Uchaguzi wa nafasi ya kiti cha Urais walikuwa hawana wapinzani.

Kwa uchaguzi wa kugombea nafasi ya Ubunge/Uwakilishi kila jimbo lilikuwa na wagombea wawili tu ambapo wapiga kura walichagua mgombea mmoja miongoni mwao kuwa Mbunge/Mwakilishi wa jimbo husika.  Uchaguzi Mkuu ulioendeshwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa zilikuwa kama ifuatavyo:-

  1. Mwaka 1980-Uchanguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano;
  2. Mwaka 1985-Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano
  3. Mwaka 1990-Uchaguzi wa kumchaua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge wakati wa mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, Uchaguzi Mkuu waTanzania/Zanzibar uliendeshwa kwa kushirikisha wagombea wa vyama mbali mbali vya siasa vilivyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria. Uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa kuvishirikisha vyama vingi ulikuwa ufuatao:

  1. Mwaka 1995-Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa majimbo 50 na Madiwani katika Wadi 141, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge;
  2. 2000-Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa majimbo 50 na Madiwani katika Wadi 142, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge;
  3. Mwaka 2005-Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa majimbo 50 na Madiwani katika Wadi 141, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge.
  4. Mwaka 2010-Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa majimbo 50 na Madiwani wa Wadi 141, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge na
  5. Mwaka 2015- Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa majimbo 54 na Madiwani 111, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge.

Bofya hapa kupata maelezo zaidi

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii