Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Kampuni  yaUjenzi ya CRJE (East Africa Limited) ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa China imetiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Afisi ya Tume ya Uchaguzi.

Hafla ya utiaji saini ilifanyika katika Afisi za Tume zilizopo Maisara Mjini Zanzibar tarehe 29 Disemba, 2023 ambapo kwa upande wa ZEC Mkataba huo ulitiwa saini na Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina na Kwa Upande wa CRJE ulitiwa saini na Ndugu Gao Yuqi ambaye ni Meneja wa Miradi waK ampuni hiyo Afisi za Zanzibar.

Akizungumza baada ya Makabidhiano ya nyaraka za Mkataba huo Makamo Mwenyekiti waTume ya Uchaguzi Mhe. Jaji Aziza Iddi Suwedi aliuomba Uongozi wa kampuni ya CRJE kujitahidi kukamilisha ujenzi huo kwa kufuata muda uliopangwa kwa mujibu wa makubaliano.

Mheshimiwa Jaji Aziza alisema, kwa upande wa Tume ya Uchaguzi ina imani kuwa, Jengo la Afisi ya Tume litakuwa na mazingira mazuri ambapo kuwepo kwa Afisi yenye mazingiramazurikutaongezaarina bidi yakufanyakazikwawatendaji.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina alisema Ujenzi wa Jengo la Afisi ya Tume hautoathiri utekelezaji wa majukumu ya Tume ikiwemo uandikishaji wa Wapiga Kura Wapya ambao unatarajiwa kuanza Mwanzo mwa Mwezi wa Disemba, 2023 nakukamlika katikati ya mwezi wa Januari, 2024.

Alisema, Afisi ya Tume inakusudia kujenga jengo lenye gorofa nne ambalo litajumuisha kumbi mbalimbali ukiwemo ukumbi wakutangazia matokeo, eneo la Studio zaTume, Ofisi mbalimbali na vyumba vya kulala

Kwa upande wake MenejawaMiradikutokaKampuniya CJRE Afisiya Zanzibar Bw. Gao YuqialiushurkuruuongoziwaTumeyaUchaguziya Zanzibar kwakuwaaminikuwapaMradiMkubwakamahuoambapoaliahidikuwaujenzihuoutakamilikakwawakatiuliopangwa.

Ujenziwajengo la Uchaguzi unatarajiwa kuanza mara baada ya Tume kukabidhi eneo kwa Kampuni ya CRJE ambapo unatarajiwa kukamilika kwa  kipindi cha miezi 9.

 

 

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii