UCHAGUZI WA MWAKA 1957
Miaka tisa (9) kupita tangu Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binaadam dhana ya uchaguzi wa kuwawezesha watu kushiriki katika masuala ya nchi zao kwa njia ya moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao ilianza kutekelezwa katika visiwa vya Zanzibar mwaka 1957 takriban miaka 50 iliyopita wananchi wa Zanzibar walipoanza kupiga kura kuchagua wawakilishi wa maeneo sita wa kuingika katika Baraza la Kutunga Sheria (Legislative Council). Vitabu vya kihistoria vinatueleza kuwa kabla ya mwaka 1957 wakati ambao wakaazi wa visiwa vya Zanzibar walipiga kura kwa mara ya kwanza, mchanganyiko wa watu wa makabila mbalimbali ya wakaazi waliishi kwa amani na usalama mkubwa sana. Mwaka 1957 ilipitishwa sheria ambayo iliruhusu visiwa vya Zanzibar kuendesha uchaguzi kwa mara ya kwanza kwa kutumia daftari la wapiga kura. kabla ya mwaka 1957, Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar ambalo lilijulikana kwa jina la “Majilish Tashlil” (Legislative Council –LEGCO) (kwa sasa ni Baraza la Wawakilishi) lilikuwa na jumla ya Wajumbe 12. Wajumbe wote hao walikuwa wakiteuliwa na Sultani wa Zanzibar ambaye kwa wakati huo ndiye alikuwa akitawala visiwa vya Unguja na Pemba. Kutokana na mabadiliko ya kisiasa ulimwenguni mfumo huo wa uteuzi ulilazimika kubadilishwa na ikaamuliwa kuwa kati ya Wajumbe 12 wa Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar, Wajumbe sita lazima wachaguliwe na wananchi na ukaandaliwa utaratibu wa namna ambavyo wananchi hao watapiga kura na kwa utaratibu gani. Kutokana na utaratibu huo mpya, ndipo mwaka 1957 ukafanyika uchaguzi wa kwanza kabisa katika historia ya visiwa vya Zanzibar na wapiga kura wakati huo waliwachagua wajumbe wawili ambao walikuwa wanawawakilisha wananchi wa maeneo ya Mjini, Wajumbe wawili walichaguliwa kuwawakilisha wananchi wa maeneo ya ng’ambo na Wajumbe wawili walikuwa wakiwawakilisha wananchi wa Pemba. Wajumbe hao sita waliungana na wajumbe wengine sita wa kuteuliwa na kuunda Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar ambalo liliendelea kuwa na Wajumbe 12. Kwa kuwa wakati huo hakukuwa na vyama vingi vya siasa, uchaguzi huo wa kwanza wa mwaka 1957 ulishirikisha vyama viwili tu vya siasa vilivyokuwepo wakati huo. Vyama hivyo vilikuwa ni vyama vya Afro- Shirazi na Zanzibar Nationalist Party. Kwa kuwa sheria ya uchaguzi wa wakati huo iliruhusu wagombea binafsi katika uchaguzi huo pia walishiriki wagombea binafsi. Katika moja ya taarifa za mwaka za utawala wa wakati huo, uchaguzi wa mwaka 1957 ulielezewa kuwa na utulivu mkubwa katika historia ya Zanzibar. Katika Uchaguzi wa mwaka 1957 ni wapiga kura 39,833 tu ndio walioandikishwa kupiga kura.
UCHAGUZI WA MWAKA 1961
Januari mwaka 1961, wanachi wa Zanzibar walipiga kura kwa mara ya pili miaka
takriban minne baada ya uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1957.