23 Disemba 2023 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph Kazi amewataka wananchi walio timiza sifa za kupiga kura kujitokeza kuendelea kujitokeza katika zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

Mwenyekiti ameyasema hayo wakati alipoanza Ziara ya kuvitembelea vituo vya uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura wapya


Akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Thabit Idarous Faina ,Wajumbe wa Tume pamoja na Maafisa mbalimbali kutoka Tume hiyo,Jaji George Kazi amesema zoezi ambalo kwa Unguja ndio limeanza kwa Mkoa wa Kaskazini,Wilaya ya Kaskazini 'A' mpaka sasa linakwenda vizuri kwa mujibu wa Wasimamizi wa vituo vya Uandikishaji ,pamoja na Mawakala wa vyama vya siasa.

Maeneo ambayo Ujumbe huo unaongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar waliyoyatembelea ni pamoja na Tumbatu,Mkokotoni,Potoa,Kidoti,Fukuchani,Tazari ,Nungwi n.k.

Akizungumza Mara baada ya kuvitembelea vituo 13 vya Uandikishaji Mkurugenzi wa Uchaguzi,Tume ya Uchaguzi Zanzibar Thabit Idarous Faina amesema licha ya kuwepo kasoro ndogo ndogo hali kwa ujumla kazi inaenda vizuri huku akizigusia baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kutokusoma kwa Alama ya vidole na Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi kwa baadhi ya waandikishwaji, ambapo masuala yote hayo huwa yanapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Vile vile ametoa wito kwa wale wote wenye sifa na vigezo wajitokeze kwa wingi katika uandikishaji wa awamu hii ya kwanza kwa sababu maandalizi mazuri ni yale yanayofanywa mapema.

Nao wajumbe wa Tume,wamewataka mawakala, wasimamizi wa vituo na Sheha wa shehia husika kufanya kazi kwa mashirikiano na wasiwe wanazibana ama kuzificha kasoro zote zinazojitokeza kwa kuieleza Tume ya Uchaguzi Zanzibar ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Zoezi Hilo la Uandikishaji wa wapiga kura wapya wenye sifa na vigezo ambalo lilianzia kisiwani Pemba mwezi wa 12 tarehe 2 na kuanza kwa Unguja tarehe 23 Disemba 2023.
Linatarajiwa kumalizika tarehe 15 mwezi wa kwanza 2024 ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii