Elimu ya Mpiga kura

Tume ya uchaguzi ya Zanzibar inajukumu la kusimamia, kukuza na kuratibu elimu ya wapiga kura kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi Nam.4 ya 2018 iliyotungwa na Baraza la wawakilishi la Zanzibar mwaka 2018 yenye nia ya kuweka utaratibu mzuri wa kupiga kura kwa kuwachagua viongozi kwa njia ya kidemokrasia.

Sheria hii ya Uchaguzi imeipa mamlaka Tume, kusimamia Elimu ya Wapiga kura chini ya kifungu cha 4(b) ambapo jukumu hili linatekelezwa kupitia Kurugenzi ya Elimu ya Wapiga Kura, habari na Uhusiano ambayo imeundwa na Divisheni tatu ikiwemo Divisheni ya Elimu ya Wapiga Kura, Divisheni ya Habari na Maktaba.

Katika utekelezaji wa jukumu hili la  kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya Wapiga Kura .  Pia kurugenzi ya Elimu ya Wapiga Kura, Habari na Uhusiano inahusika na:

  1. Kuandaa na kusimamia programu mbalimbali za elimu ya wapiga kura zilizoandaliwa na Tume,
  2. Kutayarisha mtaala wa elimu ya wapiga kura utakaotumiwa na wadau wa Uchaguzi wanapotoa elimu ya wapiga kura pamoja na kushirikiana na wadau wa uchaguzi katika shughuli za utoaji wa elimu hiyo.
  • Kuandaa vipindi vya elimu na uhamasishaji wa wadau katika kushiriki shughuli za uchaguzi. 106(2) Mtaala wa Elimu ya Wapiga Kura kwa mujibu wa Kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki utahusu elimu ya wapiga kura,taarifa kwa wapiga kura na vipindi vya uhamashaji vya Wapiga kura.
  1. Kuandaa na kuitisha mikutano na waandishi wa habari pale Tume inapotaka kutoa taarifa kwa umma
  2. Kutayarisha jarida na machapisho mbalimbali kuhusu kazi za Tume na kuzihifadhi kumbukumbu muhimu za matokeo ya shughuli za Tume.
  3. Kujenga uhusiano wa karibu kati ya Tume na Wadau wake. Jukumu hili linatekelezwa kupitia sera ya Jinsia na ushirikishwaji wa Makundi Maalum ya kijamii ya mwaka 2015 yenye nia ya kuhakikisha Makundi yote yanashiriki katika kutekeleza haki ya kidemokrasia bila usumbufu kwa kuandaa mazingira rafiki ya utekelezaji wa haki hizo.
  • Kuendesha mafunzo mbali mbali ya makundi maalum ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu ikiwemo  kuendesha mafunzo ya matumizi kifaa maalum cha kupigia kura (tactile ballot folder) kwa Watu wasioona kiwawezeshacho kupiga kura wenyewe bila usaidizi wowote.
  • Vile vile kurugenzi hii inajukumu la kujibu na kuyatolea ufafanuzi masuala mbalimbali yanayoulizwa na wananchi juu ya uendeshaji wa shughuli za Tume ya Uchaguzi.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii