HAKI NA WAJIBU WA MPIGA KURA KATIKA UANDIKISHA NA UHAKIKI WA TAARIFA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

Kiujumla kila mpiga kura ana haki na wajibu katika mwenendo mzima wa uandikishaji na uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuwa na Daftari bora na linalokubalika.

HAKI ZA MPIGA KURA

  1. Kuandikishwa kuwa mpiga kura baada ya kukidhi matakwa ya sheria.
  2. Kupatiwa elimu sahihi inayohusiana na taratibumbali mbali na hatua za kuchukua katika uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura.
  3. Kupewa taarifa sahihi zinazohitajika ili wapiga kura wengine washiriki kikamilifu katika zoezi litakaloendeshwa.
  4. Kuweka pingamizi dhidi ya orodha ya wapiga kura walioandikishwa kwa mujibu wa Sheria.

WAJIBU WA MPIGA KURA

  1. Kwenda kituoni kuandikishwa au kuhakiki taarifa zake.
  2. Kuhakikisha kwamba taarifa zake ziko sawa na zimechukuliwa kwa usahihi katika Daftari la kudumu la wapiga kura.
  3. Kuhakiki taarifa zake katika kituo alichojiandikisha au alilopiga kura kwa mara ya mwisho.
  4. Kuelimisha wapiga kura wengine kuhusiana na mwenendo mzima wa uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura.
  5. Kutoa msaada kwa wapiga kura wenye mahitaji maalum watakaohitajia kupatiwa huduma ya uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura katika vituo.
  6. Kutoa habari sahihi bila ya kujali jinsia, umri, ulemavu, na tofauti nyengine yeyote ile ya kimaumbile.

UMUHIMU WA UWAJIBIKAJI KATIKA UANDIKISHAJI NA UHAKIKI WA TAARIFA ZA WAPIGA KURA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Kila mmoja ana wajibu mkubwa katika mchakato wa uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura katika vituo. Na endapo uwajibikaji utatekelezwa na kila mdau basi utapelekea kupata tija ifuatayo;-

  1. Kupunguza malalamiko ya wadau juu ya Daftari la kudumu la wapiga kura.
  2. Kuwafanya wapiga kura wajiamini kutokana na taarifa zao kuwa sahihi na salama.
  3. Kunapunguza malalamiko ya uchaguzi.
  4. Kupunguza vurugu wakati wa uchaguzi.
  5. Unajenga usawa na uwazi katika mchakato wa Uchaguzi.
  6. Kunalifanya zoezi la uchaguzi likubalike.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii