Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeanzishwa chini ya ibara ya 119 (1) cha Katiba ya Zanzibar, 1984. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amewateua Mwenyekiti na Wajumbe a  Tume ya Uchaguzi ya tarehe 30 Aprili, 2018  kama ifuatavyo:-

1. Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid Mwenyekiti
2. Mabrouk Jabu Makame Mjumbe
3. Jaji Khamis Ramadhan Abdalla Mjumbe
4. Kombo Khamis Hassan Mjumbe
5. Bibi Jokha Khamis Makame Mjumbe
6. Kanal Mstaafu Feteh Saad Mgeni Mjumbe
7. - Mjumbe

 

Katika Kikao chake cha kwanza, Wajumbe wa Tume walimteua  Mhe. Mabrouk Jabu Makame kuwa Makamo Mwenyekiti wa Tume.

Majukumu ya Tume ya Uchaguzi  

 Kifungu Nam 119 (9) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za Tume na  atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraz ala Mapinduzi Mhe. ALi Moh'd Shein amemteua Ndg. Thabit Idarous Faina kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kuanzia 2018.

Muda wa Utumishi wa Tume ya Uchaguzi

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Nam 119 (4)(a) Mjumbe wa Tume atasita kuwa Mjumbe  ukimalizika muda wa miaka  mitano kuanzia siku  ya Uteuzi. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kuendesha na kusimamia Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na mambo mengine yanayohusiana na Uchaguzi. Tume inaundwa na Wajumbe saba na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984 kifungu cha 119(9), Mkurugenzi wa Uchaguzi ni Katibu wa Tume.

Wajumbe walioteuliwa na Rais ni Mwenyekiti, Wajumbe wawili wanaoteuliwa na Rais kwa mashauriano na Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi, Wajumbe wawili wanaoteuliwa kwa kushauriana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, mwengine ni miongoni mwa Majaji wa Mahkama kuu na Mjumbe mmoja anachaguliwa na Rais kama atakavyoona inafaa.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii