UHUSIANO WA KATIBA YA ZANZIBAR NA SHERIA YA UCHAGUZI NA AZIMIO LA KIMATAIFA LA MKATABA WA HAKI ZA KISIASA NA KIJAMII WA MWAKA 1966

Uchaguzi wa nchi ni haki ya wananchi kushiriki katika masuala yanayohusu uongozi wa nchi yao. Dhana ya haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi ilibuniwa   na Umoja wa mataifa wakati ulipotangaza Azimio la Dunia la Haki za Binadamu la mwaka 1948( the 1948 Universal Declaration of Human Rights). Azimio hilo linaeleza wazi katika Ibara ya 21 kuwa ushiriki wa wananchi katika masuala ya uongozi wa nchi yao unaweza kuwa wa moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi waliowachagua.

Azimio hili halikuwa na nguvu za kisheria; kwa maana ya kwamba halikuwa linazifunga nchi wanachama kufuata yale yalioelezwa hata hivyo, mwaka 1966 mkataba wa kimataifa wa haki za kisiasa na kijamii ulianzishwa ili kutafsiri yale yalioelezwa katika Azimio la Haki za Bnaadamu na mengineo kwa kuzifunga nchi wanachama katika kutekeleza yaliyomo katika mkataba huu.

Mbali na mambo mengine, mkataba huo kupitia ibara ya 25 unaitambua dhana ya uchaguzi kama chombo pekee katika kuwezesha watu kushiriki moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao katika masuala ya uongozi wa nchi yao. Ibara hiyo inaelezea namna ambavyo uchaguzi utafanyika kupitia vipengele (Election Elements) vifuatavyo. Vipengele hivyo ni:-

  1. Uchaguzi wa vipindi( Periodic Elections)
  2. Uchaguzi bora (Genuine Elections)
  3. Haki ya kugombania ( Right to stand for Elections)
  4. Anaestahili kupiga kura ( Universal suffrage)
  5. Haki ya kupiga kura siku ya uchaguzi( Right to vote)
  6. Usawa katika kupiga kura ( Equal Suffrage)
  7. Kura ya siri ( Secrecy of vote)
  8. Matakwa ya wapiga kura kuheshimiwa ( free expression of the will of voters)

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kwa kiasi kikubwa imetungwa kwa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Kijamii katika mambo yanayohusu uchaguzi. Katika Ibara ya 21 (1) ya Katiba ya Zanzibar inaelezwa wazi kwamba:

“Kila Mzazibari anatakuwa na haki ya kushiriki katika mambo ya uongozi wa nchi yake moja kwa moja au kupitia kwa mwakilishi wake aliyemchagua huru” Sambamba na hiyo, Ibara ndogo ya 2 ya Ibara hiyo inaelezwa kuwa” kila Mzanzibari ana haki na uhuru kushiriki katika kufanya maamuzi katika mambo yanayomhusu yeye binafsi au taifa. Ushiriki huu wa wananchi katika mambo yanayohusu Ibara hiyo utafanyika kupitia uchaguzi ambao namna ya kufanyika kwake unaelezwa kupitia kwa sheria za uchaguzi kama zilivyoelezwa katika Katiba ya 1984 na Sheria nyenginezo. Uchambuzi wa vipengele hivyo katika Katika na Sheria ya Uchaguzi ni kama ifuatavyo:-

 Bofya hapa kwa maelezo zaidi.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii