Jaala Makame Haji- ZEC

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe.Jaji Mkuu Mstaafu Hamidi Mahmoud Hamid amewahakikishia wananchi kuwa Tume ya Uchaguzi haitomkosesha haki ya kuandikishwa mtu yeyote aliyetimiza sifa za kuwemo katika Daftari la kudumu la Wapiga kura

Akizungumza katika semina iliyowashirikisha makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Haile Selasie amesema katika kufanikisha zoezi hilo na kuona kila mtu anashiriki katika masuala ya kiuchaguzi Tume imeandaa mpango maalum ambao utawawezesha watu wenye mahitaji maalum kutopanga foleni wakati wanapofika vituoni kuandikisha na kuhakiki taarifa zao

Mwenyekiti huyo amesema watendaji wa vituo na mawakala wa uandikishaji akiwemo Sheha ambaye ni wakala wa Tume watapatiwa muongozo maalum ambao utawaelekeza kumruhusu mtu huyo ambaye katika yumo makundi hayo na ambaye anasifa na mahitaji ya kupatiwa huduma hiyo.

Akiwasilisha mada ya nafasi ya Sheria katika uandikishaji mkuu wa kitengo cha huduma za sheria KHAMIS ISSA KHAMIS amesema kazi ya uandikishaji inafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Nam. 4 ya mwaka 2018

Mkuu wa kurugenzi ya elimu ya wapiga kura, habari na uhusiano JUMA SANIFU SHEHA katika semina hiyo alieleza kuwa semina za wadau zinazotolewa na Tume katika kila mzunguuko wa Uchaguzi ni kielelezo tosha kuwa tume inafanya kazi zake kwa ushirikiano na uwazi kwa kuwashirikisha wadau katika kutekeleza majukumu yake ambayo ni sifa moja wapo ya tume huru za uchaguzi na ni kiashiria cha kuwa na kuwa na chaguzi huru za haki na za kuaminika.

Washiriki wa semina hiyo Wameishukuru Tume kwa kuendelea kuwapatia elimu juu ya masuala ya Uandikishaji pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri watu wenye mahitaji maalum mara wanapofika vituoni kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao ambapo wameishauri Tume utaratibu huo uendelee katika mzunguuko wote wa uchaguzi wmkuu wa mwaka 2020.

 

Wadau wa Uchaguzi kutoka makundi maalum ya Wanawake na Watu Wenye Ulemavu wakiwa katika Semina kuhusu Uandikishaji na Uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura iliyoandaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar katika Ukumbi wa Haile Selassie tarehe 8/2/2020 ikiwa ni muendelezo wa semina zinazowashirikisha Wadau wa Uchaguzi katika masuala ya Uandikishaji.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii