Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC),Mhe.Jaji George Joseph Kazi na Wajumbe sita akiwemo Mhe.Jaji Aziza Iddi Suwedi ambae ni Makamo Mwenyekiti wa Tume hiyo,Septemba 6,2023 na Septemba 7,2023, wamefanya ziara ya siku mbili ya kutembelea Afisi Kuu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa Afisi za Unguja ambapo walitembelea Kurugenzi,Divisheni na Afisi za Wilaya ya Mjini,Wilaya ya Kati,Wilaya ya Kusini Unguja,Wilaya ya Magharibi A na B na Kaskazini A na B  pamoja na kukagua maghala ya Tume hiyo.Katika ziara hiyo,ameambatana na Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndugu.Thabit Idarous Faina na baadhi ya wakuu wa Kurugenzi na Divisheni za Tume hiyo.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii