Na Jaala Makame Haji- ZEC

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imeanza zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi wa kugombea nafasi mbali mbali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.

Akitoa maelekezo juu ya utaratibu wa Uchukuaji na urejeshaji wa fomu za Uteuzi kwa wagombea waliofika katika Afisi za Tume kuchukua fomu Mwenyekiti wa ZEC Mhe. Jaji Mkuu (Mst.) HAMID MAHMOUD HAMID alisema Mgombea atapaswa kuzifuata kanuni za maadili ya Uchaguzi ili kudumisha amani na utulivu uliopo nchini

Jaji Mahmoud alisema katika kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za uteuzi, Mgombea atatakiwa kuwa wadhamini wasiopungua 200 kwa kila Mkoa kwa Mikoa ya Zanzibar pamoja na kulipia kiasi cha Shilingi za kitanzania Milioni mbili kwa Mgombea wa nafasi ya Kiti cha Urais, laki moja Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Elfu Hamsini kwa nafasi ya Udiwani.

Jaji Mahmoud aliongeza kusema kuwa, Mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 10 katika matokeo ya Uchaguzi atarejeshewa pesa zake na atakayeshindwa kupata chini ya asilimia kumi ya matokeo hatorejeshewa fedha hizo.

Mgombea wa nafasi ya kiti cha Uraisi wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama cha Alliance for African Farmer’s part  (AAFP) wamekuwa wa kwanza kufika kufika katika Afisi za ZEC kwa ajili ya kuchukua fomu za uteuzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kukabidhiwa fomu za uteuzi Wagombea hao walisema wataendesha kampeni za kistaarabu na kushindana kwa hoja ambazo zitapelekea kuwashawishi wanachama kuwachagua siku ya Upigaji kura.

 

Aidha, wagombea hao walisisitiza suala la kudumisha Amani na utulivu kwa kila Mgombea wakati wa kampeni, upigaji kura na siku ya matokeo

Kutoka na ratiba iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar wa nafasi ya Uraisi kupitia chama cha African Democratic Alliance (ADA-TADEA) anatarajiwa kuchukuwa fomu ya uteuzi siku ya Alhamisi ya tarehe 27/8/2020 majira ya saa nne asubuhi ambapo siku ya ijumaa tarehe 28/8/2020 saa nne Asubuhi Mgombae wa nafasi hiyo kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) anatarajiwa kuchukua fomu.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii